Mahakama ya Hakimu Mkazi Manispaa ya Morogoro imemuhukumu miaka 20 jela Mshtakiwa Ally Kigugu (38) Mkazi wa Mbwade Kata ya Duthumi Morogoro Vijijini kwa kosa la kupatikana na Nyara za serikali ambapo amekutwa mnyama Twiga
Akitoa hukumu hiyo Mhe. Theresia Kaniki Hakimu Mkazi wa Manispaa ya Morogoro amesema, kosa hilo limetendeka Julai 2023 katika hifadhi iliyopo karibu na kijiji Mbwade ambacho Mshtakiwa alikuwa akiishi.
Mshitakiwa huyu amekamatwa baada ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Askari wa Uhifadhi kufanya jitihada za nguvu na kufanikisha kumpata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
#KonceptTvUpdates