Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Migombani kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamasai waishio Zanzibar (ERETO), Ndg. Thomas Makau Lepachu na ujumbe wake kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja .
Jumuiya hiyo wamemkabidhi Mbuzi na Kondoo ikiwa ni sehemu ya rambirambi yao kwa utamaduni wao.
#KonceptTvUpdates