#CBE; Benki ya Biashara nchini Ethiopia (CBE) imetoa wiki moja kwa wateja waliotoa pesa zaidi ya walizokuwa nazo kwenye akaunti zao baada ya kutokea kwa hitilafu kwenye mfumo wa ATM wazirudishe, laasivyo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Rais wa CBE, Abe Sano amesema baadhi ya wateja waliotoa pesa za ziada tayari wamezirudisha.
Zaidi ya Tzs. Bilioni 102 zimeripotiwa kutolewa kwenye benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, huku pesa nyingine zikiripotiwa kuhamishwa kwenda benki nyingine.
#KonceptTvUpdates