Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amefika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime,Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa Leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huu.
Waziri Mavunde ametumia takribani masaa 6 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)
“Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini.
Niwapongeze pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huu.
Kwakuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu,sasa naelekeza zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho mapema tarehe 26.03.2024.
Pia hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya,wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao”Alisema Mavunde
Akitoa maelezo ya awali Mkuu wa Mkoa wa Mara *Mh. Said Mtanda* amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.
Zaidi ya watu *2000* wananufaika na mgodi huu ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera
#KonceptTvUpdates