Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kufika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, kujitambulisha, ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanyabiashara na kuahidi kuwa Kampuni yake itaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kupitia program mbalimbali za kusaidia jamii na kulipa kodi.
#KonceptTvUpdatesMkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin, akizungumza kuhusu mchango wa Kampuni yake katika maendeleo ya uchumi, alipofika kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ofisini kwake (Treasury Square)Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin (kulia), kuhusu Kampuni yake kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii, alipofika kujitambulisha, katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri (Treasury Square)Mkurugenzi wa Sera wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc Kusini mwa Jangwa la Sahara, Bi. Mesiya Mwangoka, akiwasilisha hoja mbalimbali zinazohusu biashara ya Kampuni hiyo mbele ya Mhe. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipoongozana na Mkurugenzi Mpya wa Kampuni hiyo, Bi. Michelle Kilpin (kulia), aliyefika kujitambulisha jijini DodomaKamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akifafanua jambo kuhusu Sera ya fedha wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hawapo pichani), kushoto kwake ni wajumbe wa mkutano huo kutoka Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Michelle Kilpin (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na TBL baada ya kumalizika mkutano kati yao, katika Ukumbi wa Waziri wa Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma ambapo wamejadili mchango wa Kampuni hiyo katika maendeleo ya nchi.