#RipotiYaCAG; Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Ripoti zinazosomwa na CAG kila mwaka zinachangia maboresho na kuimarisha utendaji ndani ya Serikali na Mashirika ya Umma.
Rais Samia ameeleza hayo Machi 28, 2024 akiwa anapokea Ripoti kutoka kwa CAG ya mwaka wa Fedha 2022/2023 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
“Ripoti hizi ‘za CAG’ zinazosomwa kila mwaka zinachangia maboresho au kuimarisha utendaji ndani ya Serikali na mashirika ya umma. Kwa sababu dosari zilizotolewa leo hapa tutakwenda kukaa tuzifanyie kazi kisawa sawa, turekebishe, na mwakani pengine hizi hazitojirudia, tutakuwa tumesogea.” – Rais Samia Suluhu
#KonceptTvUpdates