Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza tarehe rasmi itayohusisha mchezo namba 180 wa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 kati ya Miamba mwilili inayounda “Kariakoo Derby” yaani ni Yanga SC ya Jangwani na Simba SC kutokea Msimbazi kufuatia klabu hizo kutolewa kwenye Michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
“Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba iliyofanyiwa maboresho na kutangazwa February 2024, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa April 20, 2024 kuanzia saa 11:00 jioni na tayari Club za Yanga na Simba pamoja na Wadau wengine wa Ligi Kuu wamepatiwa taarifa zote kuhusiana na mchezo huo na maandalizi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mikubwa ya Ligi ya sita kwa ubora Barani Afrika” Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu
#KonceptTvUpdates