Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekabidhi jumla ya fedha taslimu shilingi Milioni 38 za Kitanzania kwa washindi wa vipengele mbalimbali vya mashindano ya pikipiki ya Samia Motocross Championship.
Kelvin Gabriel ndiye aliyetangazwa kama mshindi wa jumla kwenye mashindano hayo akiondoka na fedha taslimu shilingi Milioni kumi za Kitanzania ambapo Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ameahidi pia kuwashika mkono kwenye kushiriki michuano ya kikanda na Kimataifa.
Msisimko mkubwa pia umekuwa kwa ndugu pacha Yannick Allad na Manuel Allard ambao wameibuka mshindi wa kwanza na wa pili kwenye kundi la Inter Midietly, wakikiri wazi kuwa baba yao mzazi amekuwa msaada mkubwa na mwalimu wao katika kukimbiza pikipiki.
#KonceptTvUpdates