Meneja wa Benki CRDB Kanda ya Dar es Salaam Muhumuliza Buberwa ameipongeza klabu ya Yanga kwa jitihada wanazozifanya kuendeleza Soka nchini.
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitashindwa kuwapongeza Yanga kwa jitihada kubwa ambayo wameifanya kwenye maendeleo ya soka, tunayo furaha kuwatangazia kuwa tutakuwa pamoja kama mdhamini mkuu wa wiki ya Mwananchi, jambo la muhimu sana katika wiki hii kuna shughuli mbalimbali ambazo zimetangazwa jana.
Katika hayo maeneo yote tutatoa huduma zote za kibenki ikiwemo kupata kadi yako ya uanachama” Muhumuliza Buberwa
Powered by @crdbbankplc @kobemotor @vodacomtanzania @hisense_tanzania_official @betpawatanzania
#KonceptTvUpdates