Benki ya CRDB ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Biashara, ndugu. Boma Raballa, imekabidhi ripoti ya utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa Wachimbaji wakati na wadogo kwa Waziri wa Madini, Mh. Antony Mavunde, mjini Kahama.
Pamoja na ripoti hiyo, Benki ya CRDB imetoa kiasi cha pesa cha shilingi Bilioni kumi kama jumla ya mkopo ulioenda kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo. Makabidhiano ya mfano wa hundi yalifanyika mbele ya Waziri wa Madini, Mh. Antony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Anamringi Macha, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh. Mboni Mhita, Mkurugenzi wa RAGAA CO LTD, Bw. Faiz Shonouda pamoja na Bi. Semeni Malale ,Mchimbaji mdogo kutoka kakola.
Benki ya CRDB inaendelea kuwa kinara katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwa kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.