Kampuni ya TOL GASES PLC leo Agosti 29,2024 imefanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa wanahisa.
Mkutano huo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo unaolenga kutoa taarifa kwa wanahisa kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kampuni hiyo pamoja na mikakati ya kuboresha huduma zake.
Kwenye mkutano huo Bodi ya wakurugenzi wa TOL Gases PLC ilieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano kampuni hiyo imewekeza jumla ya shilingi bilioni 24.8 ambapo shilingi bilioni 16.3 Bilioni zilitokana na mkopo,…
Kupitia mkutano huo uliofanyika Mlimani City Conference Centre, mengi yameweza kubainishwa na kujadiliwa kwa kina hadi kupekekea maridhiano yalipatikana kwa mapendekezo kutoka kwa Viongozi wa Bodi pamoja na Wanahisa wake.
Baada ya kusubiri kwa miaka 21, TOL Gases ilianza kulipa Gawio mwaka 2018 na imeendelea kulipa Gawio kwa Miaka mitano mfululizo, ikigawa jumla ya Tsh 9.1 Bilioni.
Katika kipindi cha miaka mitano, Kampuni imewekeza Tsh 24.8 Bilioni katika uwekezaji mkubwa ambapo TSH 16.3 Bilioni zilitokana na mkopo, na kusababisha gharama ya Fedha ya Kila mwaka ya Tsh 1 Bilioni na Tsh 8.5 zilitokana na mapato ya ndani.
Mahitaji ya sasa ya ufadhili wa kampuni yamehitaji kurekebisha mtindo wa ufadhili wa kampuni. Kwa hivyo, Wajumbe wa Kifedha wa 2023. Uamuzi huu unaruhusu Kampuni kuwekeza tena faida zake kusaidia uwezekanaji unaoendelea na kuunda thamani ya muda mrefu kwa kampuni na Wanahisa.
Mwenyekiti wa Bodi TOL Gases PLC Harry Kitilya ameeleza juu ya maamuzi mapya yaliyopendekezwa kupitia Mkutano huo wa Wanahisa 2024.
“Mradi wa “IKAMA PROJECT (2)” unafanya kazi licha ya changamoto zinazojitokeza kama Mvua nyingi, Kukatika kwa Umeme, hata hivyo bado tunayo matarajio makubwa, kwa pamoja na Wanahisa tumekubaliana kubakisha hisa ili zitumike kuongeza thamani kampuni yetu ifikapo mwaka ujaoTutakaa kuangalia huduma zetu kwa kiwango gani zinakidhi matakwa ya wateja wetu au la” -Harry KitilyaKwa upande wake moja ya Wanahisa wa Kampuni hio Elpina Mlaki amesema “Gesi yetu ni nzuri inatoka from Natural Gas (Gesi Asilia) halafu sasahivi tumewekeza kwenye ma-truck tutaenda Migodini, tutaenda mahospitalini, na tutaenda popote pale wanapotumia “gesi”, naona hio mikakati walioiweka ambayo pia tunaingoja pia watuletee mambo mazuri” -Elpina Mlaki (Mwanahisa TOL Gases PLC)#AGM
#AnnualGeneralMeeting2024
#TolGasesPlc
#KonceptTvUpdates