Akiba Commercial Bank imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni “Twende Kidigital Tukuvushe Januari” na imewahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card, na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa kibenki.
Shukrani hizo zimetolewa Jijini Dar es salaam Januari,2025 Mkuu wa Kitengo cha Biashara; Dkt. Danford Muyango, wakati wa hafla ya kuwazawadia Washindi wa Kampeni ya droo ya kwanza ya “Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari,” ambapo wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani walipokea zawadi za fedha taslimu zilizowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao pamoja na zawadi nyinginezo.
“Kampeni ya “Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari” ilizinduliwa katikati ya Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kuvuka changamoto za kifedha za mwezi huu wa Januari kupitia zawadi mbalimbali hivyo droo hii haitaishia hapa ni endelevu”amesema Danford
Wateja walionyesha furaha na shukrani kwa Akiba Commercial Bank kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote
Miongoni mwa wateja akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa zawadi hizo, Bw. Alfayo Zephania alieleza jinsi alivyopokea kwa furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo amesema “Nilifurahishwa sana na taarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora na natoa rai kwa watu wengine kujiunga na Akiba Commercial bank ili wanufaike na mengi ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakubwa katika biashara zangu”
Naye mteja Ezekiel William alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema kuwa ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni.
Aidha Akiba Commercial Bank imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na inawasitiza waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki kwa urahisi na unafuu
Mwisho .