Dar es Salaam Julai 13,
2016-kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia
na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa
intaneti katika shule za sekondari nchini
ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.
2016-kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia
na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa
intaneti katika shule za sekondari nchini
ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.
Kama sehemu ya makubaliano hayo,
wizara itabainisha na kutoa orodha ya shule zisizo na maabara za kompyuta ili ziunganishwe na hali kadhalika kuongoza utekelezaji wa mradi wakati Tigo itadhamini maendeleo ya miundombinu katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha nyaya ndani ya madarasa na kufunga visivyotumia nyaya (LAN) na vituo vinavyofikia mtandao wa intaneti.
Alipokuwa akisaini makubaliano hayo katika
Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev, alisema, “Kupitia Idara yetu ya huduma kwa jamii hivi sasa tunatekeleza dira ya serikali ya kuibadilisha nchi kuingia katika uchumi uliojikita katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kampuni yetu imejipanga kuhakikisha shule nyingi za sekondari Tanzania zinafikiwa na mtandao wa intaneti.
“Tunajivunia
kushirikiana na Wizara ya mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha vijana na jamii kwa ujumla kuingia katika mkondo wa kidunia wa habari na uelewa, ambako watajifunza, kupanua uelewa wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali duniani.”
Berdiev aliongeza kusema, “Tigo
itaendelea kufanya kazi na serikali katika miradi mingine ya ubunifu na inayovutia ili kunyanyua maisha ya Watanzania walio wengi”.
Akiishukuru Tigo wakati wa kusaini
makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora alisema, “Ni kupitia ushirikiano kama huu ndipo tutaweza kusambaza stadi za kisasa za Tehama pamoja na uelewa kwa vijana ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazotokana na mtiririko wa mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya jamii na katika uchumi wa dunia.”
Prof. Kamuzora aliongeza, “Naipongeza
Tigo kwa utayari wake wa kujingiza katika makubaliano baina ya sekta binafasi na sekta za umma ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania na vile vile tunakaribisha wadau wengine kushiriki kuunganishwa kwa teknolojia hii.
Mradi wa kielektroniki mashuleni
(eSchools) ni moja ya miradi mkakati ya uwekezaji kijamii ya Tigo na hadi sasa Tigo imeweza kuunganisha shule 31 za sekondari za serikali na mtandao wa intaneti ikiwa na mpango wa baadaye wa kuziunganisha shule 50 kwa mwaka huu. |