Utajiri wa mabilionea wa Kiafrika unaongezeka huku Mohammed Dewji ambaye ni Mfanyabiashara kupitia MeTL Group akipata $300m katika orodha mpya ya Forbes, akishikilia nafasi ya 12.
Kulingana na jarida la Forbes la mwaka 2024 la watu matajiri zaidi Afrika, Bw Dewji, maarufu kwa jina la Mo, alishuhudia utajiri wake ukipanda kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8, na kumfanya kuwa bilionea pekee anayejulikana hadharani Afrika Mashariki na Kati.
Mo Dewji anaendelea kuwa Bilionea ambaye ameajili wafanyakazi 40,000 kwa maeneo ya Afrika Mashariki na Kati, huku ameendelea kuwa miongoni mwa Matajiri bora akitajwa kwa Miaka 10 mfululizo.
#KonceptTvUpdates