Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkuu wa masoko na mauzo Barnes Hampel wa timu ya Chelsea ya England na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 01 Februari 2024.
Katika mazungumzo yao wamezungumzia kuhusu kuitangaza Zanzibar “VISIT ZANZIBAR” katika sekta ya utalii na kuanzishwa kwa Academy za mpira wa miguu nchini.
Mtindo huo wa Nchi kujitangaza nje ya mipaka yake umeanza kuwa maarufu Duniani hasa katika kuutangaza Utalii wa ndani kwa Mataifa Mengine ili kuengeza idadi ya Watalii itakayochochea ongezeko la Mapato kwa nchi husika.
Mfano mzuri unaweza chukulia nchi ya Rwanda kupitia Nembo yao ya “VISIT RWANDA” imetumika kulitangaza taifa hilo kupitia sekta ya Michezo ambapo timu ya Arsenal ya Uingereza imewekewa lebo hio kama sehemu ya kuitangaza nchi hio kimataifa.