Mshambulizi aliyewahi kuhudumu ndani ya kikosi cha Simba SC, Moses Phiri (Akiwa na jezi nambari 25) amesini mkataba mpya na klabu ya Power Dyanamos inayoshiriki Ligi kuu nchini Zambia.
Phiri amejiunga na klabu hio akitokea Simba baada ya kipindi cha usajili wa Dirisha Dogo Kukamilika kufuatia maamuzi ya makubaliano yaliyofanyika kwa pande zote mbili na kupewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu hio.
Licha ya kuwa majeruhi kwa muda kabla ya kurejea uwanjani, Phiri aliweza kuipachikia Simba mabao mengi ambayo yaliifanya Simba kumaliza nafasi ya Pili msimu wa 2022/23.
#KonceptTvUpdates