Uongozi wa Simba SC umethibitisha kwa umma kuwa umemsamehe Mchezaji wake Clatous Chama baada ya wiki chache nyuma kumsimamisha kazi kwa muda usiojulikana kufuatia kilichosemwa amekuwa na utovu wa nidhamu hivyo iliwalazimu nyota huyo afikishwe katika kamati ya nidhamu ndani ya klabu hiyo kutolea uamuzi.
Leo Februari 2, 2024 asubuhi klabu hio imetangaza kusitisha uamuzi huo baada ya kamati ya ufundi kupitia maelezo ya barua ya chama na pia uamuzi wa Benchika kumsamehe.
Chama ataungana na Kikosi cha Simba SC kilichopo mkoani Kigoma kwajili ya mchezo wake dhidi ya Mashujaa FC utaochezwa Februari 3.
Klabu ya Simba imesema itaendelea kuwekea mkazo ustawi wa nidhamu kama nguzo ya kuijenga timu bora.
#KonceptTvUpdates