Klabu ya Young Africans imesaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Pikipiki kutoka India “HERO” kwa muda wa miezi 18.
Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said ameeleza bayana katika hafla ya utiaji saini na kampuni hiyo.
“Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero” Eng.Hersi Said
#KonceptTvUpdates