JESHI la Polisi mkoani Kigoma,limemkamata mtu mmoja (29) (jina limehifadhiwa) anayedaiwa kuwa ni askari feki wa Jeshi la Polisi Tanzania, akiwa na sare zinazofanana na za jeshi hilo ambazo ni jungle green pea mbili zikiwa na cheo cha Mkaguzi wa Polisi (INSP) na kofia mbili zikiwa na nembo ya jeshi hilo.
Akizungumzia tukio hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Filemon Makungu amesema mtu huyo alikamtwa na askari waliokuwa katika doria eneo la Burega manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kupewa taarifa na wasamaria wema ambao walimtilia mashaka na baada ya kumkagua walimkuta na sare za jeshi la hilo.
Cc; Nipashe
#KonceptTvUpdates