Shirikisho la Soka Barani Afrika, limemteua Mwamuzi wa Soka, Ahmed Arajiga kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha Mashindano ya All African Games yatakayoanza kutimua vumbi Machi 8, 2024 Nchini Ghana.
Pia, Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki michuano hiyo na baadhi ya mataifa mengine kama Morocco, Senegal, Ghana, Algeria na Benin.