Balozi Shaibu Said Musa – Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amezungumza na Wahariri wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Kwenye maelezo yake ametolea ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyozuka kufuatia Sanamu lililozinduliwa Ethiopia ili Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwa kuwa na mtazamo kuwa sio muonekano halisi wa Mwasisi huyo.
“Serikali imefuata maelezo ya kitaalamu yaliyotolewa na Kamati maalum ya Wataalamu ambayo ilishiriki mjadala na mpaka kupatikana kwa sanamu, sanamu ile ilifadhiliwa na SADC kwa wazo ambalo lilitokana na Viongozi wakiongozwa na Mugabe wakati wa uhai wake kuhusu namna ambavyo watamuenzi Mwalimu Nyerere, kama tunavyojua Tanzania chini ya Uongozi wa Mwalimu tulikuwa mstari wa mbele kuongoza mapambano ya Uhuru wa Afrika, SADC wakaona na AU kukubali liwekwe lile sanamu”
“Kamati ilihusisha Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Familia ya Mwalimu Nyerere akiwemo Madaraka Nyerere, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuanzia hatua ya awali mpaka hatua ya mwisho sanamu kukamilika Kamati iliridhika”
“Kamati iliridhika kwa vigezo gani?, cha kwanza Mwalimu mnayemuona katika sanamu ile ni Mwalimu anayeelezwa wa miaka 60 mpaka miaka 80 wakati yupo active katika mapambano ya kuleta Uhuru na maendeleo katika Nchi za Afrika, pili kauli ya Mwanae Madaraka Nyerere ameitoa mara kadhaa na mpaka siku ya uzinduzi nilikuwepo Addis ameendelea kusisitiza yule ni Baba yake na kama kuna anayebisha amuulize yeye na mkitaka kumuhoji mnaweza kumtafuta” ameeleza Naibu Waziri Balozi Shaibu.
#KonceptTvUpdates