#TANZIA Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 Jioni katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya Ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo leo ambapo amesema Mzee Mwinyi alikuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na matibabu Katika Hispitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam
“Ndugu wananchi, kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, ambaye amefariki dunia leo Alhamisi tarehe 29 Februari mwaka 2024 saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.”
Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo hicho.
#KonceptTvUpdates