Baadhi ya maeneo Duniani watanufaika kushuhudia tukio adhimu la kupatwa kwa Jua siku ya leo tahehe 8 April 2024, ambapo kuanzia majira ya saa 9 jioni Mwezi utakuwa katika awamu yake ya mwezi mpya, na utaonekana kwa umbo kubwa.
Mwezi utapita mbele ya Jua na kusababisha kivuli kirefu, chenye mwendo wa haraka katika uso wa Dunia. Tukio hili linatarajiwa kuonekana katika maeneo ya Mexico kusini-magharibi hadi Newfoundland, Canada kaskazini-mashariki.
Tukio hilo limepewa jina la ‘Great American Eclipse Part II’, kwa sababu Marekani ilipata kushuhudia tukio kama hilo mwaka wa 2017. Lakini hili linatarajiwa kuwa bora zaidi pengine kwa sababu watu wengi zaidi wana uwezekano wa kushuhudia tukio la wakati huu.
Inafikiriwa baadhi ya raia milioni 32 wa Marekani wataweza kutoka nje ya nyumba zao kutazama mchana kuwa usiku.
Lakini kuna tahadhari: Kamwe, usiangalie moja kwa moja kwenye Jua bila kitu cha kukukinga. Ni hatari sana na inaweza kuharibu macho yako vibaya. Kumbuka kuwa salama.
Je, mwezi unasonga kwa kasi gani?
Kivuli kirefu cha Mwezi, kinatabiriwa kutambaa kwenye uso wa Dunia kwa zaidi ya 2,500km/h (1,500mph).
Hiyo ni takribani mara mbili ya kasi ya sauti na kasi zaidi kuliko risasi iliyofyatuliwa kutoka kwa bastola.
Kwa mujibu wa NASA, vivuli vya kupatwa vinasafiri kwa kasi ya 1,100mph kwenye ikweta na hadi 5,000mph karibu na nguzo za Dunia.
Chanzo; BBC Swahili
#KonceptTvUpdates