Mchezaji wa Zamani wa Singida Fountain Gate FC Gadiel Michael rasmi amejiunga na Cape Town Spurs FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
Imekuwa ni kitambo kidogo tangu Nyota huyo atangazwe na Klabu yake aliyohudumu zamani kuwa ameuzwa kwa Spurs ili kuweza isaidia Singida FG kupata mapato ya kuiendesha klabu kiujumla na ukizingatia inapitia changamoto ya Madeni kwa baadhi ya Wachezaji wake kwa mujibu wa FIFA kulingana na kesi za madai ya malimbikizo ya Mishahara na Ada za Usajili.“Hakuna Matata and greetings from Tanzania!, Gadiel Kamagi, Tanzanian International, has become an Urban Warrior! #Welcome to the Urban Warriors, Gadiel!” imeandikwa na @CapeTownSpursFC
KonceptTvUpdates