Kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Media, Msanii Shetta amefunguka kuhusu mahusiano yake na mama watoto wake kwa watoto wao na kwanini amesalia na watoto hao kama mlezi pekee anayeonekana kuwa karibu nao sana.
“Nimebahatika kuishi na watoto wangu. Nipo Mimi, watoto na dada wa kazi kwa miaka takribani Minne sasa. Niliondoka kwa mama yao niliwaacha watoto kwa mama yao. Nilikwenda kuishi mwenyewe baadae ndio nikaletewa watoto niishi nao kwa mapenzi ya mwanamke mwenyewe kutokana na situation ya maisha na makubaliano. Kwa sababu hata tulivyoachana tuliachana kwa makubaliano. Kwahiyo sikupata mshikemshike sana” @officialshetta
#KonceptTvupdates