Na
Krantz Mwantepele , Kahama
Krantz Mwantepele , Kahama
Utoro ni tabia ya kuondoka au
kutokufika mahali mara kwa mara bila ya kutoa taarifa. Tabia hii ipo kwenye
maeneo ya makazini pamoja na shuleni. Katika baadhi ya kata za wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.

Tabia hii imekuwa kero kwa
wanajamii wa kata za Nyandekwa na Kilago kwa kuwa inawarudisha nyuma
kimaendeleo. Wakiwa kama sehemu ya wananchi wa kata hizo, waraghbishi wamekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha watoto watoro wanahudhuria shuleni.

Ikiwa kama sehemu ya uraghbishi,
kutambua changamoto zinazokabili jamii wanayoishi, waraghbishi walitambua
kwamba hili ni tatizo na hivyo kuamua kulishughulikia.

“Nikiwa njiani kuelekea kwenye
shughuli zangu, nikakuta watoto wamejibanza kwenye kichaka, na wengine walikuwa
wakicheza mpira. Nikataka kujua kulikoni mbona hawapo shuleni, wakati ni muda
wa masomo?”

Hili
ni swali ambalo raia mwamilifu na mraghbishi Paul Izengo toka katika kijiji cha
Nyandekwa kilichopo wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, alitaka kulipatia majibu
yake. Udadisi huu ndio uliopelekea kwa yeye kuwasogelea watoto ambao kimsingi walitakiwa
kuwa shuleni mda huo na kutaka kujua kulikoni.

jibu lilikuwa ni moja tu kwamba wametoroka shule na kwanini watoroke. Paul
hakuishia tu kujiuliza maswali, alikwenda hatua moja mbele kwa kuwafuata watoto
wale na kuwauliza,

“Nyinyi
mnafanya nini hapa? Wakati huu ni muda wa kuwa darasani. Haya shuleni haraka,
niliwakaripia, hao wakakimbia.”

Kukimbia
wakati umeulizwa ni dalili ya kuogopa kutokana na kosa unalojua umefanya.
Watoto wale walijua kwamba wamekosa, na kosa lilikuwa ni utoro shuleni. Hili si
tatizo tu la kijiji cha Nyandekwa, hata Kilago pia ambapo baadhi ya wazazi
wanatajwa kuwa chanzo cha tatizo hilo la utoro.

Akiwa
kama raia mwamilifu na mraghbishi toka katika kijiji cha Kilago, wilayani
Kahama Mathew Charles anasema:

“Wazazi
ndio sababu ya utoro huu mashuleni, wanawapa watoto wao kazi muda ambao ni wa
kwenda shule. HIvyo unapomwambia ukweli anachukia anaona kama vile unamwingilia
maisha yake,”

Tabia
hiyo ya baadhi wa wazazi kuunga mkono utoro wa watoto wao kwa visingizio vya
kutaka kuwa huru na maisha, haviwatakatishi tamaa waraghbishi hao. Kwani hili
ni jukumu lao katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao.

Katika kusadia watoto
hao wanarudi shuleni, waraghbishi kupitia mtandao wao wa wilaya ya Kahama,
wamekuwa wakitoa elimu na kuwakishirikisha baadhi ya wazazi wa watoto hao
kutambua umuhimu wa elimu na inapobidi kukamata watoto watoro na
kuwapelekashule. Na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafuata na kuomba ushauri
wanapoona mtoto ameanza kuwa na tabia ya utoro. Na mara nyingi wamekuwa
wakiwashauri wazazi hawa kushirikiana na walimu ili kuweza kufuatilia maendeleo
ya watoto wao. Akifafanua hilo Michael Mathew anasema:

“Kwa mfano katika
kipindi cha mwezi wa 10 wazazi wawili wamekuja kuniomba niongee na watoto wao
umuhimu wa kwenda shule. Na nafarijika kuona harakati zangu za uraghbishi
zinatambuliwa kwenye kijiji change.

Raia Waamilifu, Mathew Charles
(kushoto) wa kijiji cha Kilago na Alphonce Peter toka kijiji cha Ufala wilayani
Kahama wakifurahia jambo walipkuwa wakijadili tatizo la utoro mashuleni

Tukiacha
hili za wazazi kutowapeleka watoto wao shule kwa sababu mbalimbali, ambapo serikali
imekuwa ikiwachulia hatua kali za kisheria wazazi hao, watoto wenyewe nao ni
chanzo cha kingine cha utoro mashuleni. Wengine wanaaga wamekwenda shule lakini
ukweli ni kwamba hawafiki shule na badala yake wanajificha wanapokujua hadi
muda wa kurudi unapofika nao hurejea majumbani kana kwamba wanatoka shule.

Hivyo
ni wajibu wa raia mwamilifu na aliye mraghbishi anapaswa kuhakikisha watoto
wanapata haki yao hii ya msingi ya elimu. Na hivyo ikibidi hata kutumia nguvu,
kama anavyosimulia Mathew Charles:

“Muda
mwingine nawabeba kwa nguvu watoto hadi shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu.
Nimeshafanya hivyo kwa watoto watano sasa. Tunajua kwamba wasiposoma sasa
watakuwa mizigo kwenye jamii. Kuna siku watatukumbuka kwamba tulikuwa
tunawasaidia,”

Ni
dhahiri kwamba tatizo hili ni kubwa na si jukumu la walimu peke yao?

Nikiwa katika picha ya pamoja na waragahbishi na raia waamilifu wa kijiji cha Kilago wilayani Kahama siku za hivi karibuni |
Kila
mwananchi pale alipo ana jukumu la kuhahakisha huduma bora za jamii
zinapatikana kwa mustakabali wa maendeleo yao. Katika kufanikisha hili raia
waamirifu ama waraghbishi toka katika vijiji vya kata ya Nyandekwa na Kilago wameonesha
njia katika kuhakikisha wanafunzi watoro wanahudhuria shuleni.

Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini
Akielezea jinsi alivyoamua
kushughulikia tatizo hilo kijijini pao, Paul ambaye pia ni kiongozi wa
waraghbishi wapya kutoka kijiji cha Nyandekwa anasema:

“Nililazimika
kumpigia simu mwalimu mkuu na kuomba kuonana naye kwa lengo la kujadiliana naye
kuhusu hili tatizo. Na pale ndipo nilipoweza kuelewa ukubwa wa tatizo la utoro.
Hivyo nikakubaliana na mwalimu kuwa tutasaidiana katika kuhakikisha kwamba
watoto watoro wanahudhuria shuleni.”

Kwa
mujibu wa orodha aliyokabidhiwa mraghbishi Paul Izengo na mwalimu mkuu wa shule
ya msingi Nyandekwa, kuna wanafunzi 21 ambao wameripotiwa utoro kati ya 449 wa
shule hiyo.

Kitendo
hiki cha mraghbishi kuamua pasipo kulazimishwa na mtu kufuatilia suala la utoro
wa wanafunzi katika shule yao ya msingi pale kijijini, ndicho ambacho raia
mwamilifu anatakiwa kukifanya.

Raia
mwamilifu ni yule ambaye anachukua hatua kwa kushirikiana na wanajamii wengine
wa maeneo yake. Huyu ni yule anayetambua majukumu na haki zake kwa mujibu wa
ibara ya 12 hadi 24 ya Katiba ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni raia anayependa
kuona mabadiliko chanya kwenye jamii yake. Huyu ni yule anayetenda pasipo
kulazimishwa, bali kwa utashi na uelewa wake kwa mujibu wa sheria na taratibu
zilizowekwa.

Katika
kuhakikisha anaelewa vizuri chanzo cha tatizo hilo, ilimlazimu Paul kwenda
kumtembelea mzazi ambaye mtoto wake yumo kwenye orodha wa watoro. Na huko
alitaka kujua, nini hasa kinachosababisha tatizo hilo.

“Nilikwenda
kwa mama mzazi wa mmoja wa wale watoto walioripotiwa kuwa watoro. Lengo langu
nilitaka kujua nini hasa tatizo mpaka mtoto haendi shuleni. Ndipo nilipogundua
kuna changamoto kubwa zaidi. Inahitajika elimu ya ziada kutolewa,”

Mama
mzazi huyo, alimweleza mraghbishi huyo kwamba michango kwa ajili ya kulipia
mitihani ya watoto wake waliopo darasa la 4 na la 6 ni changamoto kubwa
inayomkabili. Kushindwa huko kuwalipia watoto wake gharama hizo kumepelekea kwa
watoto hao kurudihswa nyumbani.

Sababu
nyingine anayoitaja mama huyo ni upungufu wa chakula hasa watoto wanapokwenda asubuhi
na kurudi shule mchana. Hali hii inasababisha watoto wasiende shule na kujikita
katika shughuli za kuzalisha kwa ajili ya familia.

Pamoja
na changamoto hizo, bado raia huyu mwamilifu alimshauri mama huyo kwenda
kuonana na mwalimu mkuu ili aangalie ni kwa jinsi gani anaweza kusaidiwa ili
watoto wake wahudhurie shuleni.

Ushauri
huu unatokana na ukweli kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo Ramadhani Masatu naye
pia ni raia mwamilifu kwa nafasi yake. Uwamilifu huo unaelezewa na mraghbishi
Elizabeth Ngayalina, toka kijiji cha Nyandekwa:

“Mwalimu
mkuu ni muelewa na ndio maana amekubali kushirikiana nasi. Ametupatia kwanza
idadi ya wanafunzi ambao ni watoro kwa kuwa anajua ni jukumu letu sote si la
kwake na walimu wenzake”

Nikiwa katika picha ya pamoja na Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini |
Kwa
hakika raia hawa waamilifu toka katika vijiji vya Nyandekwa na Kilago
wanahitaji kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo. Elimu ni haki ya msingi ya
kila mtoto na ndio maana sera ya serikali ni kutoa bure elimu ya msingi na ile
ya sekondari. Njia pekee ya kumkomboa mtoto ni kumpatia elimu ambayo ndio dira
ya maendeleo ya kila nchi, kuwa na wasomi wengi kadri iwezekanavyo.

CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO